Liwali wa jimbo la Kivu ya kusini Jean Jacques Purusi apanga kukutana na raia wa jimbo lake, hîi juma pili tarehe 8 septemba 2024. Itakuwa kwenyi uwanja wa kandanda La Concorde mjini Bukavu.
Raia walio wengi waalikwa kwa mkutano huo. Hapo liwali wa jimbo Jean Jacques Purusi ataeleza kuhusu uongozi wa jimbo. Yaani matumizi ya pesa alizozikuta ndani ya mfuko wa serkali, na zile zimeingia mfukoni humo tangu achukuwe madaraka sawa liwali wa jimbo.
Kila mtu ataruhusiwa kutowa swali kuhusu uongozi wa jimbo. Naye liwali atatowa majibu kwa wote wanaopenda kujuwa jisi anaongoza jimbo.
Mukumbuke kwamba liwali wa jimbo Jean Jacques Purusi, aliahidi kutowa ripoti mbele ya raia siku zilizopita, akiwa mbele ya wanabunge wa jimbo la Kivu ya kusini. Aliahidi pia hayo mbele ya wandishi habari, wakati wa maandamano iliyoendeshwa na wachuuzi wa soko za mji wa Bukavu.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.