Goma: Wachaguliwa washauri wa mitaa wadai serkali mishahara  ya miezi kumi

Wachaguliwa washauri wa mitaa ya Goma na ya Karisimbi wameonekana hii juma nne tarehe 22 oktoba 2024, mbele ya ikulu ya liwali  jimboni Kivu ya kaskazini, wakipiga goti. Hawa waomba serkali kuwalipa mishahara ya miezi kumi. Tangu walipochaguliwa sawa washauri wa mitaa hadi sasa hawajapokea  mishahara yao.

Moja aliyehojiwa na wandishi habari anena kwamba hali hiyo inasababisha njaa ndani ya jamaa zao. Kwa kuwa waliweza kuacha kazi zao, wakitumaini mishahara toka kazi ya ushauri, ila hakuna kinachofanyika.

Walikuwa mbele ya ikulu ya liwali wakipiga wengi , wakichukuwa mabango, ambako inaandikwa kwamba wanadai walipwe mishahara yao ya miezi yapata kumi.

Wengi miongoni mwao walisema kuwa tayari kulala usiku mahali hapo, hadi wapate jibu mhimu toka serkali, kwa kuwa hawataweza kufanya kazi, pasipo kupokea mishahara yao.

Wachaguliwa hawa wakionekana mbele ya ofisi ya liwali asubui, walikuwa wenyi huzuni mkubwa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire