Ni karibu wiki moja tangu risasi kutopigwa kiholela mjini Goma saa za usiku hasa, kama ilivyo desturi mjini humo jimboni Kivu ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Raia tuliokutana nawo wanena kwamba tangu miezi chungu tele wasumbuka na milio ya risasi muchana hasa usiku, ambayo haiwaruhusu kufunga macho. Miongoni mwa warugaruga hawo wenyi kumiliki silaha, wamoja wajipenya ndani ya nyumba za wakaazi wamoja. Wakipora mali, kujeruhi n’a hata kukuwa.
<< Imekuwa desturi siku nyingi hapa mjini Goma na kando kando tukisikia ngoma ambazo ni milio ya risasi, saal za jioni ndani ya kata za mji na kando kando. Sisi kama vile raia tunakuwa tukijiswali, akina nani ambao wapiga risasi kiholela miezi chungu tele, ijapo kuweko kwa vyombo vya usalama mjini Goma. Tangu hali hiyo kuanza, hakuna hata kiongozi kuangazia raia kuhusu heka heka inayosikika mjini jioni kama vile usiku. Nafasi nyingi kando kando ya mji, mfano wa wilaya ya Nyiragongo, askari jeshi wamoja wakiitwa wazalendo, waonekana kuzurura. Je? Hawa ndio wasababisha usalama mdogo ama wanahusika na kutekeleza usalama. Na akina nani wafyatuwa risasi eneo ambamo askari hawo wapatikana?, >>anena mkaaji huyu tuliyemhoji.
Kwa wadadisi wa mambo, labda ni kutokana na msako ambao umekamilishwa na mea wa mji , ndiyo hali kurudi tulivu siku hizi. Wakiomba hatuya hiyo iendelee bila kukoma, ili kutekeleza usalama mjini Goma na kando kando.
Tukumbushe kwamba ni tangu siku kadhaa mea wa mji wa Goma alianza kuonyesha mbele ya raia wale wanaozaniwa majambazi wenyi kusababisha usalama mdogo mjini Goma na kando kando usiku kama mchana.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.