DRC : Sheria ya nchi yatarajia Seth Kikuni kifungo cha miaka tatu

Kesi yake Seth Kikuni îmefika ukingoni hii juma tano tarehe 20 novemba 2024 kwenye jela kuu Makala mjini Kinshasa.

Mahakama ya Amani mjini Kinshasa/ Gombe yatatowa uamzi kulingana na sheria tarehe 27 novemba 2024. Mwanasheria wa serkali àomba muamzi kuelewa kwamba Seth Kikuni ameanguka ndani ya kosa yaani ukosefu wa heshima kiraia na kutapanya habari za uongo akihotubia wafwasi wa chama chake mjini Lubumbashi. Wakati huo, akiomba wafwasi wake kuondoa woga, akihakikisha kwamba Raisi wa taifa azaniwa wizi kwenyi uchaguzi.

Upande wa wanasheria washauri wake Seth Kikuni, huyu hana kosa lolote lile . Ni kazi yake kuweza kuzungumza na wafwasi wake. Masemi yake hayawezi kuchukuliwa kama makosa. Na kuomba aachiliwe huru bila shaka.

Tukumbushe kwamba ni tangu tarehe 28 oktoba 2024, ndipo kesi yake Seth Kikuni ilianza, huyu akiwa prezidenti wa chama Piste pour l’émergence. Kabla ya kufungwa ndani ya jumba la vyombo vya usalama. Huyu alishikwa tarehe 2 septemba na vyombo vya ujasusi mbele atolewe kwa muamzi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire