Habari toka Jimbo la Ituri ni kwamba watu arubaini na saba ndiyo wamefariki dunia kwenye jela kuu la Mambasa tangu mwanzoni mwa mwaka 2024.
Shirika nyipya la raia wilayani Mambasa lanena kwamba hiyo ni kutokana na hali mbaya ya wafungwa ndani ya jela hilo la Mambasa . Mratibu wa shirika nyipya la raia la Mambasa mwanasheria Jospin Paluku anena kwamba kisa cha mwisho ni hapo jana juma tatu, wakati kijana moja mwenyi imri wa miaka ishirini na mbili alifariki dunia. Akiwa hospitalini wiki moja baada ya kupewa matibabu.
Chanzo kamili ya vifo hivyo mwakani ni kutojihusisha na wafungwa ndani ya jela anena mwanasheria huyo, ambaye ni mratibu wa shirika nyipya la raia wilayani Mambasa.
Huyu àomba wanganga husika na matibabu ndani ya jela kuhusika na wafungwa sawa sawa na watu wengine. Akiongeza kwamba wafungwa wengine hufariki kutokana na hali ya uchafu ndani ya jela, ukosefu wa tiba na wa chakula.
Kwa viongozi wa jela, mwanasheria Jospin Paluku àomba kujihusisha na hali ya wafungwa, kwa kuwa miongoni mwa wafungwa arubaini na saba waliopelekwa hospitalini ajili ya matibabu, hakuna hata moja aliyeweza kupona.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.