Raisi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo angojewa mjini Kalemie hii juma nne tarehe 26 novemba 2024. Huko ataendesha kongamano ya 11 ya maliwali wa Jimbo za DRC.
Mkutano utaanzishwa juma tano tarehe 27 novemba ukilenga uongozi bora wa majimbo ili kutekeleza umoja wa makabila. Na kikao hicho cha 11 ambacho maliwali hukutana, ili ya kuzungumza kuhusu hali wanamo ongoza majimbo wenyewe kwa wenyewe.
Habari toka ofisi yake Raisi wa taifa, kazi hiyo inaambatana na katiba ya nchi, katika kipengele cha mia mbili na inafanyika mara pili kwa mwaka. Akiongeza kwamba Raisi wa taifa atahotubi raia kwenye uwanja wa kandanda Sendwe. Akikutana baadae na kundi za raia na hâta viongozi wa serkali.
<<Kikao cha maliwali wa Jimbo hufanyika mara pili kwa mwaka ndani ya kila Jimbo kulingana na matakwa yake Raisi wa taifa. Huku maliwali wanakuwa wakichambuwa mambo kuhusu namna wanazoziongoza majimbo, kisiasa na hata kisheria. Wakichukuwa mbinu kuhusu mipangilio mipya ya kazi >>ndivyo yajulisha katiba ya nchi.
Ijapo kufanyika kwa vikao hivyo, raia walio wengi hunena kwamba hakuna matokeo bora kwao kuhusu pendekezo zinazokuwa zikichukuliwa vikaoni humo ya maliwali kwa uongozi wa Raisi wa taifa.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.