Hali ilikuwa ya heka heka pa Ndosho mtaani Karisimbi usiku wa juma nne kuamkia juma tano tarehe 27 novemba 2024. Mtu moja anayezaniwa mzalendo apoteza maisha katika vurugu hiyo.
Duru za mahali zanena kwamba, ni watu wenyi kumiliki silaha miongoni mwao raia na wengine wenyi kuvaa sare za kijeshi, ndiyo walijaribu kupora ndani ya nyumba kando kando ya ofisi ya kata Ndosho mtaani Karisimbi.
Ndipo walizuwiliwa na walinzi wa usalama ambao walinasa watu saba miongoni mwa warugaruga hawo. Duru zaongeza kwamba mtu alipoteza maisha ndani ya kasoro ni mlinzi wa afisa moja mzalendo wa mahali. Vitendo kama na hiyo i
vikiripotiwa huko Nyarubande katani Kyeshero na hata Mugunga.
Shirika la raia Karisimbi laendelea kulaumu vitendo kama na hivyo, ijapo kuweko kwa uongozi wa dharura jimboni Kivu ya kaskazini. Likiomba viongozi kulinda usalama wa raia na mali yao. Wakaazi pamoja na miungano za mahali waomba uhusiano kati ya viongozi wa serkali na raia, ili kubadili mbinu kuhusu ukingo wa raia jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla na mjini Goma kwa peke.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.