Goma: Baada ya mauaji ya watu wawili, sheria yatowa uamzi

Ngoyi Inabanza akiwa wa ranka ya premier sergent wa kitengo garde républicain amehukumiwa kifungo cha kifo na mahakama ya kijeshi ijumaa iliyopita kwa kusababisha mauaji mbili.

Kifungo cha kifo, huyu akifanya ukiukaji wa kanuni na miaka 10 ya kifungo kwa kisambaza vifaa vya vita.

Huyu aliweza fyatuwa risasi kwa mwendesha pikipiki Mihigo Kalegamire na mteja wake, kwenye bandari la Goma tarehe 23 novemba iliyopita.

Askari jeshi huyo ahukumiwa kulipa wahanga pia kuhudumia vilio vya marehemu wawili.

Upande wa wahanga, mwanasheria Munguakomkwa Safari mahakama ya kijeshi ilitumia kipengele cha saba kinacho husu sheria ya kijeshi, ambacho kinampa muamzi uwezo wa kuchagua malipizi kwa hali ya juu, yaani kifungo cha kifo.

Tufahamishe kwamba kesi ilifanyika kwenye jumba kubwa la shirika SNCC kwenye bandari la Goma tarehe 29 novemba 2024.      

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire