Tangu tarehe 9 desemba hadi tarehe 22 desemba 2024, kanisa Sinaï Temple mjini Goma linaandaa mkutano mkubwa ajili ya kuhitimisha mwaka 2024, na kuingia mwakani 2025. Katika mada:<< kurejesha vitu vilivyopotea>>
Kutokana na Nabii Christian Nganzu kiongozi wa kanisa hilo mjini Goma, hayo ni kulingana na matokeo mabaya ambayo hujitokeza kila mwisho wa mwaka zaidi.
<< Unajuwa kila mwisho wa mwaka, kuna matokeo mengi sana yaliyo mabaya zaidi. Kulingana na hayo, tunaandaa mkutano mkubwa wa maombi kwa kuhitimisha mwaka. Pia ni mkutano wa marejesho kwa vitu ambavyo tulivipoteza katika hali ya ulimwengu wa roho. Inawezekana kuvipata tena vile tulivyo vipoteza, kupitia maombi na kupitia mkutano hii>>, anena Nabii Christian Nganzu.
Akizungumza na mwana ripota wa la rondeinfo.com kuhusu tofauti kati ya mkutano huo na mikutano mingine ambayo amekwisha kuandaa, Nabii Christian Nganzu atamka yafwatayo:
<< Tofauti ni kwamba katika hii mkutano tutaombea nchi yetu ya Kongo. Mungu akomeshe matatizo ambayo yapatikana ndani. Tutaombea viongozi wetu wa nchi, jeshi letu, polisi yetu. Ya zaidi tutakuwa tumeomba pamoja na kanisa kuhusu maisha ya kawaida ambayo watu wanapitia. Tofauti ni kubwa kabisa, kwa sababu vitu vingi vitaonekana kuwa vipya, vitafanyika mkutanoni. Tofauti na mikutano zingine ambazo tumefanya ndani ya mwaka. Najuwa ni mkutano mkubwa ya mwisho ya mwaka,>> asisitiza Nabii Christian Nganzu.
Akiwaalika watu wote bila ubaguzi wowote ule, watu wa dini zote ambao waamini tu kwamba Mungu anaweza akasaidie . Zaidi watu ambao wanakuwa na shida; wagonjwa, wenyi shida kikazi, watu wenyi kufungwa, familia ambazo zilifungwa na shetani kupitia matatizo kadhaa.
<<Tunaalika watu wote kwani neema ya Mungu itawagusa na itawasaidia>>, aongeza Nabii huyu wa Sinaï Temple Christian Nganzu. Akitowa ujumbe kwa raia wa Jimbo la Kivu ya kaskazini na wote wa ulimwengu mzima. << Ujumbe tunao, ni kwamba tujiunge pamoja katika mpango wa maombi. Hata kwa watu walio mbali, tujiunge pamoja kimaombi. Tukiomba pamoja ajili ya mwaka ujao, tukijiunga pia ajili ya mkutano. Najuwa Mungu atafanya mambo makubwa>>, akikomesha mazungumzo na media yako la ronde info
Tufahamishe kwamba kanisa Sinaï Temple lapatikana kwenyi kata Majengo ana kwa ana na jumba Kin marché ya huko Majengo mtaani Goma.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.