Wanamugambo FDLR pamoja na upinzani wa nchi ya Rwanda wameomba mazungumzo na nchi hiyo, Ni katika kibarua walichokituma kwake Raisi wa Angola Joâo Laurençon tarehe 22 novemba 2024. ijapo hali ya uhusiano kukwama kati ya nchi ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Tangu mwaka 2001, wanamugambo FDLR elfu 12 tayari wamerejeshwa nchini mwao Rwanda, Ila harakati hiyo yaonekana kukwama, kulingana na hali ilioko kati ya nchi hizo mbili Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Rwanda ikisisitiza kuhusika na usalama wake , anena balozi wa zamani wa Rwanda nchini DRC Vincent Karega.
Upande mwengine wanamugambo M23 waomba pia mazungumzo na serkali ya DRC, ambayo ilitupilia mbali ombi hilo. DRC ikiita kundi hili magaidi na viongozi wamoja kati yao wamekwisha hukumiwa na mahakama ya kijeshi nchini.
Ijapo hapo mbeleni mawaziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na ule wa Rwanda walisahini makubaliano ya kutaka kutekeleza amani nchini mwao, mbele yake Raisi wa Angola Joâo Laurençon. Katika lengo la kusaka wanamugambo ma FDLR nchini DRC na upande mwengine kurudisha jeshi la Rwanda nchini mwao. Ila hali yaendelea kuzorota.
Kufwatana na hayo, kazi za kufwatilia juhudi za kutaka kutafuta amani kwenye uwanja wa mapambano ziliundwa mjini Goma, miongoni watu toka pande husika, Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na wengine kutoka Angola.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.