Habari toka wilayani Lubero , zanena kwamba mkowa Matembe wilayani humo waonekana kuanguka mikononi mwa magaidi M23 hii juma pili tarehe 15 disemba, baada ya mapigano makali eneo hilo. Milio ya silaha nzito nzito ikisikika.
Duru zenyi kuamimika zaeleza kwamba ni siku kumi ya mapigano mfululizo, ndipo mkowa Matembe wilayani Lubero kuanguka mikononi mwa adui. Hali ambayo yapelekeya raia walio wengi kukimbia maskani yao, hadi nafasi ya msongano Huku wakijikuta ndani ya maisha mabovu kwa kukosa lakufanya.
Hâta shirika za kiutu kushindwa kuipeleka msaada kwa wahanga, kwani hakuna namna ya kukaribia nafasi ya mapigano. Duru zaongeza kwamba waasi wa M23, tayari wameweka vifaa vya kijeshi eneo ambalo wamekwisha kuzibiti pamoja na vikosi vyao ili kuchunga nafasi hiyo.
Mapigano hayo yaanza wakati mazungumzo kati ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pa Luanda nchini Angola haikufanyika tena. Ijapo Angola ambayo ni mahali pa mazungumzo ilingojea kikao hicho hakikutekelezwa. Rwanda ikisisitiza kuwasaka wanamugambo FDLR nchini DRC. Pamoja na hayo mazungumzo yatekelezwe kati ya waasi M23 na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Jambo DRC yatupilia mbali.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.