Kivu ya kaskazini : Shirika la kutetea haki ya walimu SYECO 2 linapanga mgomo mwanzoni mwa januari 2025

Shirika la kutetea haki ya walimu SYECO 2 Kivu ya kaskazini lapanga kuandaa kufanya mgomo tarehe 5 januari 2025 hapa karibuni, ingawa serkali ya DRC haitowe suluhu kuhusu ahadi kwa walimu.

Baada ya kufanya kikao mjini  Butembo, na kucunguza kwamba hadi sasa hakuna kilichofanyika tangu kusimamishwa kwa mgomo ya walimu wa shule za msinji na hâta zimoja za sekondari za serkali, shirika SYECO 2 Kivu ya kaskazini laona muhimu kurudilia mgomo mwezi januari 2025 hapa karibuni. Ijapo ni karibu miezi miwili, ndiyo mgomo wa kwanza ulidumu mwanzoni mwa mwaka wa shule.

Shirika la kutetea haki ya walimu SYECO 2,  laomba ilipwe sawa sawa marupurupu,  yaani prime de gratuité kwa kimombo na hâta mishahara ya walimu. Kulipa mishahara kulingana na mahali yaani zone salariale kwa kimombo yakomeshwe

Ijapo waziri husika na mambo ya élimu alikuwa tayari ametekeleza mpango mpya wa kazi mwaka huu wa shule, kulingana ha hali ya mgomo uliyodumu karibuni miezi miwili, mwanzoni mwa mwaka wa shule. Akipanga hata kalemda ya mutihani wa serkali.

Wadadisi wa mambo wanahofu kwamba mgomo mwengine ukianza, kuna hatari kubwa mwaka wa shule 2024-2025 uweze kuvunjika , na hiyo ni ukiukaji wa haki ya mtoto katika kipengele cha 43 cha katiba ya DRC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire