Goma:  Vyombo vya habari kwa njia ya mtandao Nature.cd kwa ushirikiano na Au pic naturel vyaazisha kampeni ya kupiganisha vyombo aina plastik

Vyombo vya habari kwa njia ya mtandao, Nature.cd kwa ushirikiano na Au pic naturel vyaazisha  kwenye shule Saint Michel d’Huart mjini Goma,  kampeni ili  kupiganisha matumizi ya vyombo vya plastic. Zaidi wanafunzi mia mbili wa shule hilo walihamasishwa kuhusu matatizo kuhusu matumizi ya vyombo hivyo,  na jisi ya kuhamasisha wengine, kwani vinaharibu mazingira na hata afya ya binaadam.

Denise Kyalwahi mtetezi katika sekta ya mazingira pia mratibu wa Nature.cd anena yafwatayo : Léo tulianza mpango wa kampeni ya maadibisho kuhusu mazingira kwenye shule. Katika lengo ya kukomesha vyombo vya aina plastic, tulianza kwanza kwenye shule. Na ndiyo maana tunapatikana kwenye shule la sekondari, ila tutaelekea pia kunako shule za msinji muda utakapo ruhusu. Tunataka wanafunzi hawo wapate kuhamasisha wazazi wao na hâta marafiki kuhusu hatari matumizi ya vyombo vya aina plastic, kwa kuwa vinaharibu akili ya binaadam. Ndiyo maana twaambia wazazi kwamba wasiendelee kuwapa  watoto chakula cha moto ndani ya vyombo vya aina hiyo , kwani ni kuharibu akili na hâta kusababisha maradhi kwa watoto. Jambo la pili ni kwambia watu kama vyombo vya aina plastik vinaharibu mazingira, udongo, hata nafasi ya kilimo, maji na nyama ziishimo, samaki na kadhalika. Tunapotupa vyombo vya plastic kwenye ziwa, anena Denise Kyalwahi.

Akiongeza kwamba sherti walimu nawo waelimike kuhusu ukingo wa mazingira,  kwani wanao ujuzi wa kufunza haraka watoto kuhusu kulinda vema mazingira katika somo zao. Na kwamba wamechagua kwanza shule Saint Michel d’huart kwa kuwa walimu wa shule hilo wajihusisha sana na habari za mazingira. Akihitimisha kwamba shule zingine zinaalikwa, kwa kuwa kazi itadumu muda wa miezi sita.

Upande wake kiongozi wa shule la sekondari Saint Michel d’Huart Divin Ombeni anena kufurahi kuchaguliwa wakwanza kuhusu kampeni.<< Kama munavyo fahamu, mazingira ni binaadam na yote inayomuzunguka. Kwa kuwa watoto wetu wapatikana ndani ya jamii, ni hawo wataweza kusambaza habari ndani ya jamii, wakihamasisha wenzao kuhusu ukingo wa mazingira. Mjini Goma watu hawajali habari kuhusu ukingo wa mazingira, ijapo  huwa wahanga wa matokeo mabaya ya kutokinga mazingira. Tutadumu katika kazi hizi tukiunda klabu ambayo itahusika na kuchambua mada dhidi ya mazingira,>> anena kiongozi wa shule hilo.

Asisitiza kwamba klabu hiyo itadumu. Na kwamba itakuwa ikishuka kila mara uwanjani,  ili kuhamasisha raia na hâta shule zingine. Kwa kuwa kuwa shida ni chungu tele kuhusu ukingo wa mazingira mjini Goma. Na kwamba sherti wanafunzi washike kazi hiyo na mikono miwili na mambo yatabadilika mjini.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire