
Wafanya kazi wa shirika husika na volkeno , OVG mjini Goma wamechukuwa hatua ya kusimamisha mgomo, ambao imedumu miezi kumi na miwili.
Walikusudia hayo katika kikao hii juma tatu tarehe 13 januari 2025. Asilimia hamsini ya madai kuhusu marupurupu maalum yalijibiliwa na serkali ya DRC.
Wafanya kazi hawo waligusia mambo mengi wakati wa kikao. Mfano ya uhusiano bora kati yao, kuzidisha juhudi za utetezi kwa kuepuka rushwa, kushikana bega kwa bega kwa kudai serkali haki yao, kuepuka hali ya uchochezi mbele ya viongozi wao, kutupilia mbali hali ya fitina na kadhalika.
Wakizungumza ana kwa ana, waliambiana kweli, wakinena kupiganisha hali ya magawanyiko wenyewe kwa wenyewe. Baadae prezidenti wa kutetea haki ya wafanya kazi wa shirika OVG Zirirane Bijandwe Innocent alishukuru viongozi wa serkali waliojihusisha kutafuta suluhu kwa shida ya wafanya kazi wa shirika OVG.
<< Tunasema asante kwake liwali wa Jimbo ambaye usiku na mchana alijihusisha kutafuta suluhu kwa shida yetu. Mbele ya yote Raisi wa taifa ambaye alisikia malalamiko yetu na kutuandalia marupurupu maalum, kwa kuwa tunao mishahara mdogo. Bila kusahau waziri mkuu, pamoja naye waziri Kabanda ambaye alitembelea widhara ya feza na kadhalika, ili tupate jibu mhimu. Tunasimamisha mgomo kwa muda, tukiamini kwamba muda wa mwezi moja, serkali ataweza kujibu, kwa kuwa nusu ya marupurupu yetu imebaki>>, amena Bwana Zirirane Bijandwe Innocent baada ya kikao.
Wafanya kazi walisema kufurahi na jambo lililofanyika, wakichukuwa hatua ya kusimamisha mgomo, na kuomba serkali kufanya haraka iwezekanayo Ili kutimiza mara moja ahadi.
Tukumbushe kwamba ni miezi kumi na miwili sasa tangu wafanya kazi wa shirika OVG walianza mgomo, wakidai serkali kulipa marupurupu maalum, iliyo ahadi yake Raisi wa DRC kwao.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.