DRC : Shirika husika na pesa ulimwenguni FMI latowa bilioni 3 dola za marekani kwa DRC

Shirika husika na pesa ulimwenguni FMI lanena kuunga mikono DRC, katika mipangilio kiuchumi na kipesa kwa dola bilioni 3 za marekani.

Hayo yalihakikishwa naye waziri nchini husika na uchumi pia pesa Doudou Fwamba hii alhamisi tarehe 16 januari 2025 wakati wa mkutano wa mawaziri mjini Kinshasa.

Shirika husika na pesa ulimwenguni FMI laonyesha uaminifu kwa uongozi wake Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo. Milioni 240 itatumwa mbele ili kuhakikisha kutumwa kwa pesa zingine, ambazo zitatumwa baadae. Na zitatumiwa katika miradi mhimu,  mfano ya ujenzi.

Waziri husika na uchumi pia pesa Doudou Fwamba anena kufwatilia matumizi bora ya pesa hizo, Ili ya kutekeleza mendeleo ya kudumu.

Upande wake kiongozi mkuu makamu wa shirika husika na pesa ulimwenguni FMI, ambaye pia ni prezidenti wa shauri la uongozi wa FMI, pesa hizo zitasaidia DRC kutatuwa shida kwa sasa, na kuzidisha nguvu, kusaidia katika kupiganisha mazingira, kwa kuwa DRC ni nchi suluhu ulimwenguni kuhusu kuchafuka kwa mazingira.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire