Goma : Liwali wa Jimbo Carly Nzanzu Kasivita anena kuwa ugonjwa wa Corona haujakoma na inabidi mcango wa wote kwa kuupiganisha

Liwali wa Jimbo la Kivu ya kaskazini alikutana hii juma tano tarehe 7 aprili na waandishi wa habari mjini Goma akigusia zaidi hali ya usalama mdogo unaokumba Jimbo lake na kuweko kwa ugonjwa wa Corona ambao umesababisha vifo zaidi ya mia tatu tangu kuripotiwa Jimboni kwenyi jumla ya visa 2242 , watu 1737 wakipata uponyaji.

Kwake liwali kuongeza kwa visa vya ugonjwa wa Corona kunatokana na uhusiano kati ya Jimbo la Kivu ya kaskazini na nchi za Rwanda na Uganda ambazo zachangia mipaka na Jimbo hilo, bila kusahau uwanja wa ndege wa Goma ambao unarahisha mawasiliano na ulimwengu mzima

« Inabidi raia kujuwa kwamba ugonjwa wa Corona uko na ni hatari kwa maisha ya kila moja. Inabidi mcango wa wote ili kuipiganisha , kila mtu akivaa vizuri barakowa , kunawa mikono na kujitenga » anena liwali wakati huo.

Akiongeza kwamba Kivu ya kaskazini ni ya pili ndani ya Jimbo zilizokumbwa zaidi na virusi vya Corona , Kinshasa ikichukuwa nafasi ya kwanza ikiwa na visa 20344.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire