Kivu ya kaskazini : Siku kuu ulimwenguni ya mazingira Mratibu jimboni husika aalika wote kutunza mazingira

Siku kuu ulimwenguni ya mazingira, Uratibu husika na mazingira jimboni Kivu ya kaskazini umeanza kazi ya kuondoa uchafu kwenyi soko kadhaa mjini Goma, Mfano wa soko ya Kituku ambako kazi za kuondowa uchafu zilianzishwa kinaganaga hii tarehe 21 juni 2023. Baada ya naibu wa liwali wa jimbo kuanzisha rasmi kazi hizo, akipanda miti kwenyi mlima Mont Goma. Namna ya kuonyesha raia kwamba liwali wa jimbo ameweka mkazo kwa siku kuu hiyo, ambayo alitaka ifanyike tarehe 20 hadi 23 juni 2023 , ikiitwa << juma la mazingira.>>

Matamshi ni yake Mratibu jimboni husika na mazingira Kivu ya kaskazini Jean Flavien Baseme , akihojiwa na mwana ripota wa la ronde info kwenyi soko ya Kituku hii tarehe 21 juni 2023.

<<Ilikuwa fursa kwetu kuondoa uchafu ndani ya soko ya Kituku. Tukitaja nafasi ya machinjio, nafasi ya wavuvi na kadhalika, ila kazi zinaendelea.>> Aeleza kiongozi huyo.

Akihojiwa kuhusu kuondoa uchafu ndani ya soko zingine mjini na kandokando ambazo kunajaa uchafu, Mratibu jimboni husika na mazingira Jean Flavien Baseme anena kwamba soko hizo ni zenyi kuwa na viongozi husika. Na kwamba raia hulipa ushuru kuhusu kazi za usafi. Inabidi pesa zinazolipwa kutekeleza usafi,

Ijapo hiyo Bwana Jean Flavien aongeza kwamba swala la ulinzi wa mazingira litafwatiliwa kwa makini kote jimboni. Akisisitiza kuwafunza raia kuhusu ulinzi wa mazingira. Huyu awaomba kutotupa uchafu ovyo ovyo barabarani, kwa kutoharibu mazingira. Na kwamba atakaye naswa astahili malipizi. Kwa kila mkaaji kutunza uchafu nyumbani kwake ama kuiweka kwenyi nafasi inayostahili, ili ya matumizi yake. Ama kujiorodhesha kwenyi shirika zihusikazo na kuondowa uchafu mjini.

Tufahamishe kwamba Mratibu jimboni husika na mazingira alisindikizwa na wasaidizi husika na sekta hiyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire