Goma: Bwana Adolphe Mweze auliwa kwenyi barabara Mutinga

Bwana Adolphe akiwa dreva kwenyi shirika la kimataifa la msalaba mwekundu CICR ameuwawz jioni ya juma pili tarehe 31 machi mwaka huu pa Mutinga barabara kuelelea Majengo mjini goma. Akifyatuliwa risasi na watu wasiojulikana.

Duru za mahali zanena kwamba dreva huyu aliuliwa na watu wanaozaniwa kuwa Wazalendo. Hawa walikuwa ndani ya gari, wakimushutumu kuwa chanzo cha msongamano ndani ya barabara. Ndio kumfyatuliya risasi na kufariki hapo hapo.

Tukumbushe kwamba usalama mdogo inapanda mnara siku kwa siku mjini goma . Wakishotwa vidole katika kazi hiyo haramu wanamugambo Wazalendo pamoja na vijana askari jeshi mjini Goma .

Juma lililopita msichana alipoteza maisha kwa kupigwa risasi kutokana na vuta ni kuvute kati ya askari jeshi wawili katani Majengo hapa mjini Goma.

Juvénal Murhula.