Kivu ya kaskazini : Liwali wa Jimbo aahidi maendeleo ya wilaya ya Walikale

Liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini Constant NDIMA arudi mjini Goma toka Walikale ambako alitembelea mara ya kwanza tangu achukuwe madaraka ya Jimbo la kivu ya kaskazini.

Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege, huyu anena kuwa alienda jioneya binafsi jisi hali ilivyo huko kiusalama na hata kutoendelea kwa wilaya hiyo.

Pamoja na raia walichukuwa hatua ya kujihusisha na maendeleo ya eneo hilo la kivu ya kaskazini.

Na kuhusu wanamugambo wenyi kumiliki silaha kinyume na sheria, liwali anena kuwa amejielekeza kwenyi makao ya kijeshi ili kuona waliojisalimisha . Akiahidi raia kujionea wenyewe kuhusu wale wasiopenda jisalimisha wenyewe.

Upande wake mwanabunge Prince Kihangi mcaguliwa wa Walikale anena kufurahishwa na hatua yake liwali , kujielekeza makwao. Na kwamba hii ni matakwa yake Raisi wa DRC Felii Antoine TSHISEKEDI. Mwanabunge huyu asisitiza kuwa kutoendelea kwa wilaya ya Walikale tangu mbeleni ni moja wapo wa nia mbaya ya viongozi wamoja wa serkali.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire