Akitokea mjini Goma, mwanabunge wa taifa nchini DRC Patrick MUNYOMO amekutana hii juma mosi na wandishi habari wengi wa mji wa Goma. Huyu anena kujihusisha na wenzake upande wa Muungano Union sacrée ili serkali ivunje haraka iwezekanayo ushuru RAM ambayo yasumbuwa raia wakongomani.
Mcaguliwa huyu anena kuwa wametuma kibarua kwake waziri ahusikae na mawasiliano ili kuondowa ushuru huo na kufasiria nini pesa kutokana na ushuru wenyewe zimefanya.
N’a kwamba waziri ajibu kuwa swala halimuhusu peke yaani serkali ya DRC nzima.
Akijibu moja kwa moja kwa maswala ya wandishi habari, yeye alinena kufwatilia kinaganaga ujenzi wa barabara Kilijiwe ambalo kazi zitatekelezwa hapa karibuni, bila kusahau barabara 1 km, yote kwa manufaa ya wachaguzi wake.
Pamoja na hayo, kuondowa na matumizi ya jezi ndani ya ziwa Kivu ambayo ni hatari kwa raia jimboni Kivu ya kaskazini na kusini. Wakati huo Patrick MUNYOMO atembelea waziri ahusikae na mafuta ya petroli na kuhakikisha kuwa ni dola mia tano elfu za marekani ndizo zimetolewa kwanza na serkali kuhusu swala hilo.
Na mwishowe swala la walimu ambalo afahamisha kuwa walimu wa kianglikani na hata wa kimbangu jimboni watapokea mishahara hapa karibuni kutokana na utetezi wake. Mwanabunge MUNYOMO atajielekeza mjini Kinshasa pamoja na watetezi na walimu ili kufwatilia shida zao. Mfano ya walimu wapya, walimu wasiolipwa, na hata kuongezea wengine mishahara.
Juvénal MURHULA
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.