
Ma mia ya akina mama waja wazito na watoto wadogo walala nje siku hizi pa Pangi jimboni Maniema kutokana na mvua kali ziliyonyesha huko mwanzoni mwa juma.
Duru zenyi kuaminika toka eneo hilo zajulisha kwamba ni nyumba zaidi ya 191 ndizo zilibomoka kutokana na mvua hizo n’a vijiji tano ndivyo viliguswa na ajali.
Wahanga wa ajali hiyo waomba serkali ya jimbo na hata ya taifa kujihusisha na swala hilo. Waomba pia mtu yeyote wa moyo mwema na hata mashirika za kiutu kuwahudumia kwani waendelea kulala nje wakikosa msaada.
Tufahamishe kwamba mvua hizo zilisindikizwa na upepo mkali ambayo ilisababisha maafa mengi eneo hizo za jimbo la Maniema.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.