Goma : Liwali wa jimbo ashurtisha waorodheshwe wageni kila leo mjini

Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Peter Chirimwami aomba mea wa mji kuchukua hatua ili kuorodhesha kila wageni mjini. Ili kurahisha vyombo vya usalama kufanya vizuri kazi yao. Wakichunguza watu wanaoingia na kutoka mjini Goma jimboni Kivu ya kaskazini. Kwani mji wa Goma unakumbwa na hali ya wasi wasi kutokana na vita vinavyo sababishwa na watenda maovu wa M23.

Hiyo ni hatua iliochukuliwa ndani ya kikao kuhusu usalama hii juma tano tarehe 31 januari 2024. Ambayo ilihudumiwa naye liwali wa jimbo, makamu wake, mea wa mji, kamisa wa jimbo Kapend Kamand Faustin pamoja viongozi wa tabaka za chini mjini Goma.

Liwali wa jimbo alilazimisha mea wa mji kutowa kila leo ripoti ili ya kujua akina nani waliingia mjini na kuwa na uhakika kuhusu hali yao ndani ya mji.

<<Inabidi tukae pamoja ili kupiganisha usalama mdogo mjini Goma. Inabidi kila saa nne mbele ya mchana kati tupate ripoti kuhusu wageni wenyi kupatikana mjini. Ili kurahisishia vyombo vya usalama kufanya vizuri kazi yao. >>Akihotubia raia, liwali mwanajeshi. Péter Chirimwami alilaumu pia hali ya usalama mdogo kila leo mjini Goma na kando kando yake.

Wakieleza malalamiko yao mbele ya liwali, viongozi wa tabaka za chini, walieleza ukosefu wa maji safi kwenyi eneo kadhaa mjini , utumizi mubaya wa maji ya mvua na hata ukosefu wa moto wa umeme, ukosefu pia wa mwangaza kunako barabara.

Kwa hiyo, mea wa mji aliahidi kwamba vyombo vya usalama pamoja na raia watajihusisha na swala hilo. Akiomba raia kwa jumla kujihusisha na hali ya usalama ili ya kugunduwa maadui wa amani mjini Goma.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire