Goma: Mwili usio na uhai wa kitoto kichanga umegunduliwa pa Ndosho

Mji wa Goma.

Mwili wa kitoto kichanga usio na uhai umekutwa asubui ya juma tatu pa Ndosho huko Rwasama mtaani Karisimbi.

Claude Rugo prezidenti wa vijana mtaani Goma anena kwamba mwili huo wa miezi karibu miwili uligunduliwa na wapita njia.

« Hatujuwe aliyetupa mwili huo ndani ya shimu yenyi mita 15, inabidi ucunguzi ili kugunduwa mtenda maovu huyo. Inawezekana ni akina mama ambaye alichokoza mimba » anena kiongozi wa shauri la vijana Claude Rugo.

Habari ilihakikishwa naye kiongozi wa kata Ndosho ambaye aliahidi uchunguzi. Mazishi yalifanyika hapo hapo kwa ruhusa ya viongozi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire