Shirika la raia lahuzunishwa na kuvamiwa kwa vijiji vingi vya eneo hilo na wanamugambo Mai mai. Hali inayo sababishwa na ukosefu wa askari jeshi FARDC.
Bwana Georges Katsongo wa miungano ya shirika la raia aomba askari jeshi kutekeleza usalama eneo, ili kupanguza machozi maelfu ya raia, wanao sumbuliwa na kundi hizo zenyi kushikilia silaha.
« Tulitazama tangu wiki iliyopita kundi hizo zenyi kutembea kusini hadi kaskazini. Ngome nyingi zimekwisha kujengwa ndani ya vijiji vingi upande wa Kinyatsi eneo la Masumo, Musasa, Makoko, Viyunga na nafasi zingine pa Mabambi. Popote kundi hizo zapatikana, raia hawaelewe kwa nini hiyo, » alaumu Georges Katsongo.
Duru zetu zaeleza pia kwamba wa mai mai Nduma walivamia kempi ya askari jeshi pa Vuyinga, tangu tarehe 20 julai mbele ya kushambuliwa na waasi wa Mazembe siku hiyo. Wanakaa hapo kwa kuwa hakuna askari jeshi FARDC. Upande mwengine kundi lingine lilivamia kempi ingine ya jeshi ya Byambwe, eneo la Manzia wilayani tu Lubero.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.