Kananga: Akina mama saba wamefariki dunia na moja apatikana katika hali maututi wakipigwa na radi

Wanawake munane wamepigwa na radi hii juma tano tarehe 3 agosti majira ya saa saba, wakati wa mvua iliyo nyesha dakika kumi. Hayo yalifanyika kwenyi soko Ofida, kata Kamayi, mtaani Kananga huko Kasaï ya kati.

Duru zenyi toka Kasaï ya kati zaeleza kwamba akina mama hayo walipigwa radi wote kwa dakika moja wakati wa mvua iliyonyesha dakika kumi peke.

Duru zaongeza kwamba akina mama saba tayari wameaga dunia, moja kati yao akiwa katika hali maututi.

Tufahamishe kwamba hadi sasa hakuna anayefahamu chanzo cha ajali hiyo.

Issa Félix

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire