Kivu ya kusini : Mtu moja ajeruhiwa kwa risasi pa Misisi

Habari toka pa Misisi jimboni Kivu ya kusini zaeleza kwamba, mtu moja amejeruhiwa munamo usiku wa ijumaa kuamkia juma mosi tarehe 20 Agosti 2022. Ni katika shambulizi kwa silaha.

Wevi wenyi kumiliki silaha aina Ak 47 walipenya ndani ya nyumba ya mcuuzi moja wa zahabu aitwa Bertin, kwa jina maarufu Kopao. Ni katika kitongoji Balala, sekta ya Nganja.

Jambazi hawo, ambao hesabu haifahamike vizuri walipora kiasi cha zahabu pamoja na kiwango cha pesa.

Baadae walinyatuka, wakipiga risasi kwa kujipatia njia. Duru zetu zaeleza kwamba mhanga yaani mtu aliyejeruhiwa, alipelekwa hima kwenyi kituo cha afya cha mahali, ambako anapewa tiba.

Issa Libiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire