DRC : Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anena kukerwa na hali ya nchi inayo sababishwa na Rwanda jirani

Raisi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo , afasiria kuwa na moyo mwema, akiweka mbele diplomasia, alipofika madarakani nchini.

Katika mkutano na wandishi habari mjini Kinshasa, amesema kuvunjika moyo, kutokana na hali ya usalama iliyoko mashariki mwa DRC.

« Nilipochukuwa madaraka, nilitia mbele uhusiano kidiplomasia na majirani. Nikizani kwamba suluhu itapatikana kwa mwanzo. Juweni kwamba, mimi ni wa kwanza kuguswa, na hata kufazaika kutokana na hali iliyoko nchini. Hiyo ni kutokana na nchi jirani ambayo ilipenda tutembee pamoja. Na kwa leo,nchi hiyo yana tutatiza« , atamka Raisi Félix Antoine Tshisekedi.

Huyu aongeza kwamba nchi yake yashurtishwa kutekeleza amani ; « Kwa hiyo niko nikijitahidi, »anena Raisi, akihakikisha kuchukua hatua ili kutekeleza usalama mashariki mwa DRC, akitumia mbinu zote.

Kwa hiyo, kumepita siku chache, tangu Raisi Félix Antoine Tshisekedi alihakikisha kutumwa nchini, kwa vikosi vya Afrika EAC, hapa karibuni.

« Vikosi vya Burundi tayari vimewasili nchini DRC. Ni katika lengo hilo. Kuhusu muda vikosi vyote vitaanza operesheni, watalaam wataeleza. Ya mhimu ni kwamba hatua imechukuliwa, na nguvu za pamoja zimeanza, » aeleza Raisi wa DRC.

« Haija tajwa tarehe kuhusu kutumwa kwa vikosi vyote. Watalaam wakiangazia kwamba,inabidi kujifunza hali ya uwanja wa mapambano, vifaa vya kazi pamoja na pesa, ili kufikia lengo. Upande wangu, tayari harakati zimeanza. Viongozi wa kijeshi wa kila kundi wamekwisha kutanana. Wengi miongoni mwao wamekwisha kugawa ngome, » asisitiza Raisi Félix Antoine Tshisekedi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire