Uganda: Helikopta ya wanajeshi UPDF yaanguka mkowani Kabarole

Duru toka mpakani mwa Uganda zaeleza kwamba, Helikopta moja husika na kazi za shambulizi ya jeshi ADF imeanguka hii juma nne tarehe 27 septemba kiisha mchana kati. Ni kwenyi mkowa Kabarole pa Uganda mpakani na DRC, eneo la Basongora pa Béni, sekta ya Ruwenzori, jimboni Kivu ya kaskazini.

Ndege hiyo yahusika na shambulizi katika operesheni za pamoja FARDC UPDF, dhidi ya wanamugambo ADF wilayani Beni, Irumu na Mambasa wilayani Ituri.

Duru toka hapa n’a pâle zanena kwamba hakujajulikana chanzo cha ajali hiyo hadi sasa. Ila Helikopta hiyo ilikuwa ikipeleka wanajeshi wa FARDC pamoja n’a wale wa UPDF.

Tukumbushe kwamba ni tangu mwezi novemba 2021, ndipo maraisi wa DRC na Uganda walikubaliana kutumia nguvu za pamoja ili kuwagonga magaidi wa ADF wanaozorotesha usalama mashariki mwa DRC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire