Goma: Mtu moja apoteza maisha katika ajali ya barabara kwenyi kata Mugunga

Ajali ya barabara ilijitokeza mjini Goma kwenyi barabara Goma Saké mtaani Karisimbi jimboni Kivu ya kaskazini.

Habari toka shirika la raia la huko zaeleza kwamba ni gari moja aina Canter ndilo liligonga mwendesha piki piki moja, ambaye alikuwa akielekea upande wa Sake.

« Gari moja aina Canter liligonga mwendesha piki piki moja na kufarikk hapo hapo. Wakati ule gari lilichukuwa mbio mahali isiyo julikana. Tunaomba madreva wa gari kuwa makini wanapotembeza gari zao barabarani, »  laeleza shirika la raia la Mugunga.

Tufahamishe kwamba ajali za barabarani zaripotiwa kila leo kwenyi barabara Goma Sake, ambazo zasababisha vifo vya watu n’a hata majeraha.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire