Kasaï ya kati/ Kananga: Kanisa moja la kikatoliki lashambuliwa likiporwa na kuunguzwa na vijana

Kanisa la kikatoliki Saint Eloi Bikuku pa Kananga Kasaï ya kati lilishambuliwa hii juma mosi tarehe 1 octoba 2022 majira ya saa kumi za asubui na kundi la vijana.

Padri Théophile Tshimanga akijieleza kwa vyombo vya habari anena kwamba vijana hawo, walibomowa mlango wa kanisa na kujipenya ndani. Wakipeleka vitabu vitakatifu, mavazi za ma padri. Akiongeza kwamba hata ukaristia na hata vingine viliharibiwa hata kuunguzwa.

Akihojiwa ingawa kuna mizozo kati ya ma padri na kundi hilo la vijana, huyu anena kwamba wao kama wachungaji, hawana gasia yoyote, vijana hawo ni wenyi kutambulika n’a watu wote .

« Askari polisi walitumwa kwenyi eneo, na uchunguzi umeanzishwa ili kufahamu chanzo cha shambulizi hilo, na kutowa azabu kwa wahusika, » duru zetu zaangazia.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire