Rutshuru: Vifo tatu vyaripotiwa kati ya wahami wa vita wapatikanao pa Rwasa

Watu tatu wamefariki dunia miongpni mwa wahami wenyi kupatikana kwenyi kempi Rwasa umbali wa kilomita mbili na kiwanja mtaani Rutshuru. Hayo ni kutokana n’a mizozo ya vita ya magaidi wa M23, wakiungwa mkono n’a Rwanda.

Aimé Mukanda moja wa wenyi busara wilayani Rutshuru anena kwamba, watu hawo walifariki kutokana na njaa. Akiongeza kwamba miongoni mwa watu 200 wenyi kupatikana eneo hilo, asilimia 90 ni wenyi kukumbwa na njaa. Ndipo aomba serkali kufanya iwezekanayo ili kurudisha usalama. Wahami hawo warudi kwao Jomba , kwani maisha ndani ya kempi ni ngumu mno.

Tufahamishe kwamba ni tangu mwanzoni mwa vita vyenyi kutokana na magaidi wa M23, wakiungwa mkono n’a Rwanda, wahami wa vita waongezeka kila leo, wakihofia maisha yao.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire