Zaidi ya watu 150 elfu ni Wahami pia wanyonge wilayani Nyiragongo n’a Rutshuru

Hii ni ripoti kutoka Shirika la kimataifa husika na mambo ya kiutu OCHA, na idadi hiyo hutokana na mapigano Kati ya jeshi la taïfa na waasi wa M23.

Matokeo hayo ya Uratibu wa shirika husika na mambo ya kiutu OCHA ni ripoti ya tarehe 8 hadi tarehe 14 Juni 2022

Akihojiwa ijumaa iliyopita, Kiongozi husika na mambo ya kiutu kwenyi shirika hilo tawi la Rutshuru anena kwamba hali ya wahami ndani ya wilaya hizo yaendelea kuzorota,wahanga wakiwa na woga kusaulika.
Ingrid Bokosset aomba viongozi husika kufanya yote iwezekanayo ili shirika OCHA kufikia wahanga mahali wapatikana, hasa kunako kituo cha afya cha Rwanguba. Akiomba pia viongozi kufanya juhudi ili kukomesha usalama mdogo jimboni Kivu ya kaskazini.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire