Wahami wa vita ya M23 toka wilayani Rutshuru na Nyiragongo, wamepokea chakula hii juma nne tarehe 13 disemba 2022. Walipokea mchele, mafuta, maharagwe , cumvi na unga toka mikono ya watumishi wa Mungu. Ni muungano wa makanisa za kibatisti yaani UEBCO, CBCA CBCE, CEBCO ndizo zilitowa msaada kwa wahami.
Kiongozi wa timu lenyi kuhusika na huduma Reverendi Pasta Daktari Gaston Mulera mwakilishi wa 55eme CEBCE, anena kwamba, ijapo kimwili, wahami hawo wahudumiwa pia kiroho.
« Sisi tunahudumiya wahami hawa pia kiroho. Kuko watumishi wetu ambao wanawa fundisha neno la Mungu kwenyi kempi mbali mbali, » anena Prezidenti wa timu hilo la ma pasta
Miongoni mwa wahami, kunapatikana walemavu, wamama wanyonge, wazee na hata watoto. Hawa walishukuru kwa huduma toka makanisa za kibatisti, UEBCO, CBCA, CBCE, CEBCO
Sisi tunashukuru kwa msaada huu toka makanisa za kibatisti, p UEBCO, CBCA, CBCE na CEBCO. Tunapokea mchele, mafuta, maharagwe na chumvi. Tunaomba makanisa zingine na kila yeyote wa moyo mwema, kuiga mfano huu. Serkali ya jimbo la Kivu ya kaskazini iliwakilishwa kwenyi kazi hiyo.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.