Bukavu : Mwanaume moja amefariki dunia kwa kujitundika katani Panzi

Mwanaume moja amefariki dunia kwa kujitundika katani Panzi mjini Bukavu. Hayo yalifanyika munamo usiku wa juma pili kuamkia juma tatu tarehe 26 disemba 2022.

Kiongozi wa shirika la raia mtaani Ibanda David Cikuru anena kwamba, mhanga alikuwa mwenyi umri wa miaka thelasini, alikutwa amejitundika nyumbani kwake. Ila chanzo cha kifo hakijajulikana bado.

David Cikuru aongeza kwamba jambo hilo lilifanyika kwenyi kitongoji Ruzizi ya kwanza, katani Panzi mjini Bukavu jimboni Kivu ya kusini.

Tufahamishe kwamba ni visa yapata kumi ya watu kujitundika ndivyo vimeripotiwa hadi sasa, tangu mwanzoni mwa mwaka 2022. Chanzo ya vifo bila kujilikana.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire