Nyiragongo: Jules Lubungo alaumu hali ya usalama mdogo wilayani humo

Wakaazi wa Kiziba ya kwanza eneo la Munigi wilayani Nyiragpngo walikuwa wenyi hasira kubwa, tangu usiku wa juma pili kuamkia juma tatu tarehe 23 januari 2023. Ni kutokana na kuuliwa kwa kiongozi moja na tabaka za chini kwa jina la Aksanti Jules, ambaye aliuliwa kwa kupigwa risasi na wasiotambulikana vizuri.

Bwana Jules Lubungo moja wa wakaazi wa Kiziba ya pili pia prezidenti wa kamati ya wachuuzi wa soko Alanine amesema kukerwa na hali hiyo.

« Sisi tuna huzuni kubwa kutokana na usalama mdogo unaokumba wilaya ya Nyiragpngo. Hasa kuuliwa kwa kiongozi moja wa mahali, akijaribu kutowa nafasi ambako wevi wenyi kushikilia silaha wanakuwa wakijificha. Tunaendelza kujiswali vyombo vya usalama vinafanya kazi gani yaani shirika la ujasusi, askari polisi na hata askari jeshi. Wakaazi waingiliwa na jambazi nyumba kwa nyumba kila leo, ila hakuna msaada wowote ule. Hata nyumba zaidi ya nyumba kwa siku kuingiliwa. Watu wauliwa, waporwa mali yao na Kadhalika bila msaada, » anena Jules Lubungo mbele ya wandishi habari akiwa mwenyi hasira

Huyu aongeza kwamba ingawa wakaazi waendelea kuungana mkono kwa mkono, waonekana kutoungwa mkono na serkali, na ndio sababu ya kutofaulu kutekeleza amani.

Prezidenti wa kamati ya soko Alanine aomba serkali kufanya yote iwezekanayo, ili kutekeleza amani wilayani Nyiragpngo ambako raia waendelea kuangamizwa.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire