Goma : Akina mama viongozi wa shirika FUDEI walazimisha kurudi kwa wahami wa vita makwao katika hali ya usalama

Kulazimisha wahami wa vita kurudi makwao, shurti mbele waweze kurudi kwenyi vijiji vyao na mengineo. Ndio ya mhimu iliyozungumzwa katika mkutano ya akina mama viongozi memba wa shirika lisilo la kiserkali FUDEI. Ilifanyika mjini Goma kama ilivyo desturi wakati wa kipindi cha maombi kila wiki.

Akina mama hawo wakiongozwa naye Prezidenti wa shirika lihusikalo na mambo ya kiroho pia maendeleo FUDEI Rachel Mululu. Hawa waliweza mbele ya yote kushukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi. Wakialika roho mtakatifu atawale mazungumzo tangu mwanzo hadi mwisho.

<<Tuko tukizungumza kuhusu makuu ya Mungu. Anaweza yote, atatuletea amani. Siyo vikosi vya nchi za Afrika ya mashariki ndivyo vitatuletea amani, ama vya Monusco, ama vile vya SADEC. Havita leta amani ya kudumu. Tuna kuja kumulilia Mwenyezi Mungu atuoneye huruma, atupe amani ya kudumu. Tumetowa pendekezo na hata suluhu kwa mda ambazo tutapeleka kwenyi serkali. Kwa leo tuliomba ajili ya serkali ya taifa, hasa kwa Raisi wa taifa, kwa liwali wa jimbo na kwa viongozi wengine. Ni katika lengo la kusii Mwenyezi Mungu ambaye anaweza tekeleza amani bila shaka>>, anena Bi Rachel Mululu Prezidenti wa shirika FUDEI.

Bi Rachel Mululu anena kukutana na wahami wa vita ambao pamoja wanaendelea kumulilia Mwenyezi Mungu, viongozi wa serkali, makanisa na shirika zisizo za kiserkali.

<<Tunaamini kwamba Mungu amesikia machozi yetu na pasipo mashaka tutafikia amani ya kudumu, >>anena akina mama huyo.

Rachel Mululu anena kwamba sherti majeshi ya ugenini irudi makwao, kwa kuwa imeshindwa kazi tangu miaka mingi yaani MONUSCO na hata vikosi vya Afrika ya mashariki. Na kwamba tumaini ni kwa jeshi la taifa FARDC, ambalo litaendelea na mapigano hadi kurudi kwa amani kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Upande wake mjumbe wa liwali wa jimbo alinena kufurahishwa na kazi za akina mama. Akiahidi kwamba serkali ya DRC itawasindikiza ili kutekeleza amani ya kudumu. akiahidi kufikisha pia pendekezo kwa liwali wa jimbo. Na kusisitiza kwamba jambo la usalama lahusu kila mtu. Na kwamba kuwe uhusiano kinaganaga kati ya raia na viongozi wa serkali ili kutekeleza amani, kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire