Goma: Mheshimiwa Acheni Lukwebo yupo ziarani mjini Goma ajili ya kazi

Akipokelewa kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Mheshimiwa Acheni Lukwebo Prezidenti wa chama cha kisiasa AFDPC yaani Alliance des Forces Démocratiques pour le Progrès du Congo kwa kimombo, amewasili hii juma tano tarehe 12 julai 2023 mjini Goma.

Kwenyi uwanja wa ndege, amepokelewa kwa shamra shamra na wanamemba wa chama, ambao walikuja kumlaki. Akija ili kuweka vikartasi vyake kwenyi Tume huru ya uchaguzi CENI, akigombea nafasi bungeni.

Miongoni mwa maswala, Prezidenti wa chama cha kisiasa AFDPC Acheni Lukwebo alihojiwa kuhusu jina lake ambalo limepanda kiasi mjini Goma kwa peke, na jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla.

Akifasiria kwamba kupanda kwa jina kunatokana na kazi anazo zitekeleza humu jimboni Kivu ya kaskazini. Na kwamba hii ni ushuhuda ya raia wa jimbo wenyewe.

Mengi kuhusu ziara yake humu jimboni Kivu ya kaskazini, mutaya fahamishwa katika habari zijazo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire