Kivu ya kaskazini : Willy MISHIKI apinga kukomesha haraka uongozi wa kijeshi

Akiwa ziarani jimboni humo, moja wa viongozi wazee wa mji Prince Willy MISHIKI anena kufurahishwa na hatua yake Raisi wa DRC, kwa kuandaa kikao, ili kuzungumza kuhusu kubaki ama kuondowa uongozi wa kijeshi yaani état de siège, eneo hili la DRC. Ingawa wengi miongoni mwa walio shiriki kikao wanena kwamba uongozi wa kijeshi ukomeshwe, Willy MISHIKI hakubali jambo hilo, akiomba uongozi huo usikomeshwe haraka.

<<Mimi simo miongoni mwa walio omba kuhitimisha uongozi wa kijeshi yaani état de siège kwa kimombo, kwa kuwa adui angali kwenyi mlango. Tuna haki ya kusema kwamba usalama ni mbovu hadi sasa, kwa kuwa viongozi wamoja wa kijeshi hasa ndani ya wilaya wametumika vibaya, ila siyo chanzo ya kuomba kukomesha uongozi huo. Kama itakomeshwa, ifanyike haraka,>> anena Prince Willy MISHIKI.

Huyu ana matumaini kuhusu vikosi vya SADEC na hata vijana wakongomani, ambao wamekubali kuingia ndani ya jeshi la taifa FARDC kwa kupigania nchi yao. Akiomba raia kuunga mkono askari jeshi, kwa kuwa bila raia, jeshi halina nguvu. Na kwa wale hawataki mara tena uongozi wa kijeshi, waache kushota vidole wengine wanao taka uongozi huo uendelee.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire