Goma : Mkutano kuhusu kilimo na viwanda tayari umeanza

Exif_JPEG_420

Ni hîi ijumaa tarehe 15 machi ndipo mkutano kuhusu kilimo na viwanda umeanza kwenyi jumba Full gospel mjini Goma. Walikuweko viongozi wa Muungano Maarifa, viongozi wa serkali pamoja na raia walio wengi. Zaidi ya waundaji kazi sitini walionyesha vitu wanavyo vitengeneza, ili kuweza kuvinunua, na kufikia maendeleo..

Vitu vizuri na vingi vilikuwa vimetandikwa tangu saa za alfadjiri. Navyo ni mafuta ya kupakaa, sabuni, vinywaji mbali mbali, mifuko na mikaba inayotengenezwa kwa ngozi za ngombe, shati na suruali, coffee, kwa jumla, vinywaji, mavazi na vitu vingine vya kupamba mahali

Akichukuwa usemi kuhusu mkutano huo wa kiuchumi, kiongozi wa Muungano Maarifa John KAVYAVU anena kwamba, ni namna ya kuleta mchango ajili ya kuinua uchumi mjini Goma kwa peke, na jimboni Kivu ya kaskazini na hata kwa nchi nzima. Akishuru kwa ujio wa viongozi wengi wa serkali na wale wa mashirika, waliweza kujibu kwa mwaliko na hata raia kwa jumla.

John KAVYAVU aliomba  viongozi kwa ngapi zote, mashirika hapa na pâle, na hata raia kwa jumla kusindikiza kazi hizo za waundaji kazi, kwa kuwa ni namna ya kupunguza ukosefu wa kazi, pia ni moja wa maendeleo jimboni Klvu ya kaskazini. Aliahidi kwamba mkutano huo ambao ni kipindi cha kwanza mjini Goma utaweza kutanda kote jimboni Klvu ya kaskazini na kwenyi majimbo mengine.

Moja kwa moja viongozi kadhaa walichukua usemi, wakisema kuunga mkono kazi za Muungano Maarifa, kwa kuwa ni namna ya kusaidia serkali kupunguza ukosefu wa kazi, kupunguza idadi ya kundi zenyi kumiliki silaha zikitatiza raia siku kwa siku.

Wengi miongoni mwao walishangaa na kazi hizo ambazo vijana mjini wamechapa, wakisema kushitushwa na ujuzi huo mkubwa  ambao bado kujilikana vizuri. Waliahidi kwa jumla kusindikiza hadi kufikia lengo.

Miongoni mwa viongozi hawo, mwapatikana  wale wa idara mbali mbali jimboni Klvu ya kaskazini, mwzkilishi wa mea wa mji pamoja na ule bunge jimboni.

Waundaji kazi wengi miongoni mwao walifasiria kazi wanazozifanya, wakishuru  Muungano Maarifa kwa huduma, hasa katika utetezi mbele ya serkali ili aweze kupunguza ushuru na kadhalika. Wakiomba raia kuja kununua vitu wanavyo vitengeneza kwa bei inavyofaa. Kwa kuwa wana hitaji pesa ili kuweza kuinua uchumi na kufikia maendeleo. Na kutopeleka pesa kwenyi nchi za nje, ili kutopoteza mali ya nchi.

Tufahamishe kwamba ni kesho juma mosi tarehe 16 machi ndipo itahitimishwa mkutano huo kuhusu kilomo na viwanda mjini Goma. Raia waalikwa kuja kujionea wenyewe.

Juvénal  Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire