Nyiragongo: Mtu moja auwawa eneo hilo

Watu wenyi kumiliki silaha, wasio Juliana  waliuwa mtu moja mwenyi umri wa miaka thelasini na mbili munamo usiku wa juma pili tarehe 16 juni mwaka huu.  Hayo yalifanyika kwenyi kijiji Kabaya eneo la Munigi wilayani Nyiragongo Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali zaeleza kwamba ajali ilifanyika si mbali na makao ya mhanga, kwenyi usultani Marongo. Na kwamba ni jambazi wenyi kumiliki silaha wakivaa sare za kijeshi.

Tukibaki eneo hilo la Munigi tueleze kwamba mtu mwengine anayezaniwa mwizi,  aliunguzwa kwa moto na raia kwenyi kijiji Turunga. Ni katika usiku huo wa juma pili kuamkia juma tatu tarehe 17 juni mwaka tunao.

Kulingana na hali hiyo mtaani Nyiragongo, uratibu wa shirika la raia MSCO unaomba serkali kutia mkazo kuhusu usalama eneo hilo. Kwa kuongeza idadi ya askari polisi ili kulinda raia na mali yao.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire