Goma: Mtaa wa Karisimbi wakumbwa na shida ya maji

Duru toka shirika la raia la mahali zaeleza kwamba mirija ambayo inapeleka maji imeharibika, maji humwangika  na ndio chanzo cha ukosefu wa maji.

Prezidenti wa shirika la raia mtaani Karisimbi aomba wateja wa shirika Regideso kulipa déni ili kurahisisha kazi kwa shirika lenyewe.

<<Kweli ukosefu wa maji inaonekana mtaani Karisimbi. Raia wanakumbwa na shida. Tulienda kuona viongozi wa Regideso. Nawo walisema kukumbwa na shida. Eleweni kwamba kuna shida zimoja ambazo zinasababishwa na shirika zimoja za serkali na hâta viongozi ambao hawataki kulipa déni za maji. Hîi ni shida kubwa kwa shirika la kugawa maji Regideso,>> anena kiongozi wa shirika la raia mtaani Karisimbi.

Upande wa shirika Regideso, viongozi husema kwamba wafanya kazi wajitahidi usiku na  mchana ili kutafuta suluhisho. Huku shirika likianza kubadili vyombo ambavyo viliwekwa na viongozi wa zamani.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire