Kinshasa : Ma dreva watolewa Siku kumi mbele ya kutekelezwa kwa malipo mapya kwao

Waziri husika na uchukuzi mjini Kinshasa Bob Mbisso ametowa Siku kumi kwa madreva wa shirika la uchukuzi ACCO mjini Kinshasa. Baada ya mgomo ulifanyika na  madreva hawo, wakipinga hatua ya haraka iliyochukuliwa na serkali kuhusu daftari  nyipya ya malipo ya pesa za serkali.

Viongozi wa sekta hii ya uchukuzi wakutanana ana kwa ana na waziri husika, Ili kuonyesha vinyume kuhusu hatua ya haraka iliyochukuliwa na serkali ya DRC, kuhusu mpango mpya wa malipo ya pesa za serkali.

Huku waziri husika na mambo ya uchukuzi mjini Kinshasa, kuwaomba kuhamasisha ma dreva wote, kusudi waelewe na kukubali mpango mpya wa malipo ya pesa za serkali, mbele ya kuitekeleza.

Tufahamishe kwamba mji wa Kinshasa ukiwa siku hizi katika hali ya msongano, kila dreva akijikatia beyi ya malipo mwenyewe kwa wateja wake, ilibidi serkali kujihusisha ndani ya swala. Jambo lililopelekea ma dreva mjini Kinshasa, kufanya mgomo hii juma tatu tarehe 13 januari 2025.

Juvénal Murhula.


Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire