Mashirika na Miungano husika na madini pamoja na zile za barabarani zimesahini makubaliano kwa kukarabati barabara nambari 2, Mugogo, Walungu, Mwenga. Wakikubali kutowa mchango Ili ya ujenzi wa barabara hiyo, ambayo yapelekeya kwenye wilaya ya Mwenga, jimboni Kivu ya kusini.
Hayo yalifanyika mbele ya waziri husika na mambo ya madini jimboni Kivu ya kusini, kwenye mkahawa Bodega mjini Bukavu. Ni baada ya mazungumzo uliyodumu tangu asubui juma tano hadi saa za jioni. Huku ikipelekea mashirika hizo za madini kukubali kusahini makubaliano.
Lilikuweko shirika la raia ambalo lilijihusisha na uhamasishaji, ili kazi hizo zifanyike.
Upande wa raia, inabidi kazi hizo zianze, maana kila mara viongozi wa Jimbo na hâta wale wa taifa, wanakuwa wakichukuwa mipangilio, ambayo yaonekana vigumu kutekeleza.
Tukumbushe kwamba ujenzi wa barabara hiyo ni ya muhimu zaidi kuhusu mawasiliano ya mji wa Bukavu na wilaya ya Mwenga, jimboni Kivu ya kusini. Barabara ambayo ulionekana kuachiliwa jimboni humo.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.