Raia saba wamepoteza maisha, wakiuwawa na waasi M23 kwa kulipisha kisasi, mkowani Kihondo usultani wa Bwito wilayani Rutshuru.
Duru toka huko zaeleza kwamba, wanamugambo wazalendo waliteka nyara waasi M23 na kuwateketeza. Baada ya hapo, waasi hawo kulipisha kisasi, wakiwageuza kuwa wazalendo na kuwatendea kinyama.
<< Majira ya saa kumi na moja, juma tano tarehe 15 januari 2025, mituto ya risasi ikisikika mkowani Kihondo usultani wa Bwito wilayani Rutshuru. Wazalendo wakiteka nyara waasi wa M23, na kuuwawa kiasi. Ndiyo waasi kugeuza raia kuwa wazalendo. Watu saba miongoni mwao waendesha pikipiki pamoja na wateja wao kuuwawa, na watu karibuni saba wengine kujeruhiwa>>, anena mwakilishi wa liwali wa Jimbo huko Isaac Kibira mbele ya vyombo vya habari
Duru hizi zaongeza kwamba waasi M23 wanaposhindwa katika mapigano , kila mara hulipisha kisasi kwa raia, wakigeuza kuwa maadui, pahali pa kuwakinga.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.