Goma : Carly Nzanzu Kasivita aomba raia kujiunga na viongozi wa kijeshi ili kutekeleza usalama Kivu ya kaskazini

Liwali wa Jimbo la Kivu ya kaskazini Carly Nzanzu Kasivita

Katika mkutano na wandishi habari hii juma tano tarehe 5 mei liwali wa Jimbo la Kivu ya kaskazini Carly Nzanzu Kasivita anena kuunga mkono hatua iliyochukuliwa naye Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI ili amani irudi jimboni Kivu ya kaskazini.

Liwali aonyesha kuwa hatua ya kuwakabizi madaraka viongozi wa kijeshi yaambatana na katiba ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo .

Akiomba kundi zenyi kumiliki silaha kuweka silaha chini kuondoka msituni ili ya kujenga amani. Pia vijana kusindikiza juhudi za askari jeshi ili kufikia amani ya kudumu jimboni Kivu ya kaskazini.

Carly Nzanzu Kasivita anena kuwa amani ikirudi kazi za maendeleo zitafanyika mfano utalii na mengineo.

Alishukuru vyombo vya habari kuunga mkono alipokuwa madarakani na kuomba kuendelea hivyo kwa kiongozi mpya wa jeshi atakae chukuwa madaraka.

Liwali wa jimbo Carly asema kuwa haki za kawadi zitaheshimiwa ingawa kutakuwa tofauti kidogo na wakati alipokuwa madarakani na kwamba liwali wa kijeshi atajihusisha na maswala yote kuhusu Jimbo nzima.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire