Goma: Emmanuel Gashamba aleta vikartasi kuhusu mtihani wa serkali

Emmanuel Gazhamba akuja na ujumbe toka widhara ya elimu ya kiufundi nchini DRC.

Inspekta ahusikae na elimu ya kiufundi Jimboni Kivu ya kaskazini Emmanuel Gashamba afahamisha kuanzishwa kwa mtihani wa serkali katika sekta ya kiufundi mara ya kwanza Kinshasa, Kivu ya kaskazini na kusini. Akikuja na mizigo ya vikartasi vya mutihani wa serkali. Nakufahamisha kuwa mtihani wa serkali utaanzishwa rasmi naye liwali wa kijeshi hii juma tatu tarehe mosi agosti 2021. Ni wa kandideti 1663 ndio wangojewa kwenyi mtihani jimboni na watalipa kila moja elfu 60 franka za kongo ili kufanya mtihani.

Inspekta huyu akuja na ujumbe mkuu toka sekta ya elimu ya kiufundi ili kuja kucunguza jinsi kazi zaendeshwa humu jimboni Kivu ya kaskazini na kusini, ambayo ni hitaji yake Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDi TSHILOMBO.

Kwa kuwa ni mara ya kwanza mtihani uanzishwe katika sekta ya elimu mkondo wa kiufundi ,ulieleza ujumbe mkuu toka mjini Kinshasa. N’a kufahamisha kuja kwake humu jimboni waziri ahusikae na elimu ya kiufundi nchini DRC.

Emmanuel Gazhamba ndani ya ujumbe toka mjini Kinshasa

Baada ya kukutana na ma inspekta kadhaa jimboni Kivu ya kaskazini alinena kuwa vikartasi vya mutihani wa serkali vitapelekwa haraka katika eneo mbali mbali humu jimboni ili kungojea kazi zianzishwe.

 » Tutajiandaa kutuma vikartasi vya mutihani huo Walikale ya kati yaani Biniwe, Mubi, Hombo ya kaskazini na Pinga. Mcana tu wa leo vikartasi vingine vitapelekwa haraka pa Masisi yaani Mweso na Kitchanga. Vikartasi vingine vitapelekwa Kiwanja ili kufikishwa Jomba na Nyamilima ya kati. Vingine vitabaki mjini Goma ili kungojea gisi liwali wa jimbo mwana jeshi ataanzisha rasmi kazi za mtihani kunako shule la sekondari Mwanga aeleza kiongozi huyu mbele ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege pa Goma.

Emmanuel Gashamba aomba wote ambao ni kandideti kwenyi mtihani huo kujielekeza kunako shule Mwanga siyo kwenyi shule Rutobogo kama walivyozania.

Kuhusu ukingo dhidi ya virusi vya Corona wakati wa mtihani, Inspekta Gashamba anena kwamba mipango imechukuliwa na waziri ahusikae na sekta hiyo ili kukinga wanafunzi. Akisema kuwa kila mwanafunzi atapewa barakowa mbili, kutakuwa pia dawa ya kuuwa virusi, na kuheshimu kanuni kwa kuikala.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire