Kivu ya kusini : Shirika nyipya la raia NDSCI lalaumu hali mbovu ambamo waishi watoto chini ya umri jimboni

Watoto wa mitaani chini ya umri jimboni Kivu ya kusini

Shirika nyipya la raia NDSCI Kivu ya kusini laendelea kulaumu hali ya kuzurura kwa watoto wenyi chini ya umri kwenyi soko nyinyi na eneo kadhaa jimboni Kivu ya kusini.

Katika uchunguzi uliofanyika ndani ya soko jimboni humo , wanamemba wa shirika nyipya la raia wakuta kwamba watoto wenyi chini ya umri hutumikishwa , wamoja wakiuzisha mifuko midogo midogo yaani sachets sokoni, wengine ndazi na wengine watumikishwa wakiomba barabarani.

Hawa wamekuta kwamba watoto wengine watumikishwa ndani ya nyumba za malaya na kwenyi nafasi ya uchimbaji mawe.

Shirika nyipya la raia kupitia Alfred Habamungu laongeza kuwa zaidi ya watoto arubaini wauzisha sachets kunako soko ya Brasserie, Mugogo na hata kwenyi soko kuu la Kadutu.

Na kunako soko Bondeko kwenyi Beach Muhanzi wengine waendesha vitendo vya wizi, kutumika ndani ya restaurant na wengine kutumikishwa katika vitendo vya ngono. Uchunguzi huo waonyesha kuwa hata wengine watumikishwa upande wa wavuvi na hata wilayani Kabare ndani ya soko ya Mudaka.

Wakihojiwa na wanamemba wa NDSCI , wamoja waeleza kuwa wanafanya kazi hiyo kwa kuwa ni yatima, wengine watamka ukosefu wa jamaa zao, na wengine kwamba hawaendi shuleni kwa kuwa walimu wao wapatikana mgomoni.

Hayo yapelekea shirika nyipya la raia kuomba wazazi kucunga watoto wakati huu wa mgomo ili kuepuka hatari. Na kwa wale wenyi kutumikisha watoto kuacha tabia hiyo wasije wakaazibiwe.

Na kwa mwisho NDSCI aomba wahusikao na ukingo wa watoto kutobaki nyuma kwani watoto hawa wapo hatarani.

Chumba cha uhariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire