Goma: Hali yaendelea kuwa shwari Buhumba pa Nyiragongo ambako askari jeshi FARDC wazibiti eneo

Askari wa taifa FARDC

Hali umerudi tulivu huko Buhumba wilayani Nyiragongo baada ya mapigano kati ya askari jeshi wa taifa FARDC na wale wa Rwanda waliojipenyeza kwenyi udongo wa DRC.

Shirika la raia la mahali lanena kwamba moja kwa moja raia warudi vijijini mwao ambavyo vilikuwa vimezibitiwa na askari jeshi wa Rwanda. Ila Kijiji Kabundi mpakani na Rwanda ndipo hawaja rudi wakiendelea kuhofia maisha yao.

Hawa waomba serkali kutuma askari jeshi eneo hilo ili kuwalindia usalama.

Duru zenyi kuaminika zaeleza kuwa askari wa Rwanda walifaulu kutowa wenzao wawili mikononi mwa jeshi FARDC ambako walikuwa wamefungwa.

Na kwamba askari FARDC wamefaulu kupokonya silaha moja kwa wale wa Rwanda.

Kutokana na timu la CiRGL, uchunguzi unaendeshwa ili kugundua chanzo cha hali. Hakuja ripotiwa vifo ama majeraha toka mapambano hayo.

Chumba cha uhariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire