Goma: Prezidenti wa chama cha kisiasa ADES apokelewa kwa shangwe na vigelegele

Prezidenti wa chama cha kisiasa ADES Kaboyi Bwivu Jean Bosco kwenyi uwanja wa ndege pa Goma.

Prezidenti wa chama cha kisiasa nchini DRC ADES kwa maarufu anena kuja mjini Goma ili kushimika rasmi chama cha kisiasa ADES . Akitowa hongera kwa raia wa jimbo la Kivu ya kaskazini wanaokumbwa na mauaji kila leo kutokana na usalama mdogo. Chama cha kisiasa ADES kwa kimombo Alliance des Démocrates pour l’égalité kitaleta mabadiliko bora katika maisha ya wakongomani.

Prezidenti wa chama cha kisiasa ADES Kaboyi Bwivu Jean Bosco anena hayo akipokelewa na umati kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii ijumaa tarehe 28 januari 2022.

Wanamemba wa chama hicho miongoni ma kada na wafwasi walimupokea kwa shamra shamra hadi mjini Goma ambako alihotubia raia walio wengi.

Raia ndani ya jumba la mkutano.

Kiongozi huyu akisisitiza kuhusu kuboresha hali ya maisha ya wakongomani. Na kuomba raia kuunga mkono chama hicho. Huku raia yapata mia wameji orozesha ndani ya chama ADES.

Aliyekuwa Mwanabunge wa zamani Kaboyi Bwivu ajibu baadae kwa maswala ya wandishi habari:

« Ninayo furaha kubwa kwa mapokezi makubwa na ninaamini kupitia chama cha kisiasa ADES mabadiliko yataonekana katika hali ya maisha ya wakongomani, » aeleza Kiongozi.

Kiongozi wa chama ADES akijibu kwa maswala ya wandishi habari baada ya kikao.

« Kwa raia walionipokea nawambia kwamba uchaguzi ni mwaka 2023 hapa karibuni. Waweze kuunga mkono chama hiki ili ya mabadiliko bora na ya kudumu nchini DRC« , atamka Bwana Kaboyi Bwivu Jean Bosco.

Akiomba subira kwa raia wa Kalehe chama ni kwao na kwa wakongomani wote, ijapo kimefunguliwa rasmi jimboni Kivu ya kaskazini. Kiongozi huyu aonyesha kwamba ni namna ya kupongeza raia wa jimbo hilo kupitia magumu waishimo kila leo.

Juvénal Murhula

1 Comment

Poster un Commentaire