Bukavu : Kiongozi makamu wa mtaa wa Kadutu atoa hongera kwa jamaa la kijana aliyeaga dunia kwa kufyatuliwa risasi pa Pas à pas Buholo1

Mji wa buka

Tunalaumu vitendo vya umwangaji damu, nikiahidi uchunguzi ili kugunduwa watenda maovu hawo

Namegabe Mweze David kiongozi makamu wa mtaa huo anena kuwa binafsi alipeleka mhanga wa pili alijeruhiwa katika shambulizi hilo kwenyi hospitali kuu ya Bukavu. Huyu ni mteja aliyekuwa ndani ya jumba ambamo ajali ilifanyika.

« Ni majira ya saa moja na nusu ndipo warugaruga walishambulia nyumba ndogo ya Airtel money na kufyatulia risasi kijana moja aliyefariki dunia hapo hapo. Mwengine ni mteja naye alifyatuliwa risasi na nikampeleka binafsi ndani ya gari langu kwenyi hospitali kuu ya Bukavu. Huyu ambaye bado kujulikana apatikana katika hali maututi » anena kiongozi wa mtaa wa Kadutu.

Duru zingine hueleza kwamba kijana aliyefariki dunia ni mwenyi umri wa miaka ishirini, aliyekuwa mwanafunzi kwenyi shule la sekondari Saint François Xavier pa Kadutu Biname mtaani Kadutu.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire